ZARI AELEZEA KINACHOWAGOMBANISHA ZAIDI YEYE NA DIAMOND

Katika kipindi cha Leo tena kinachorushwa na kituo cha Clouds FM kilichofanyika leo siku ya Alhamisi, wageni katika studio walikuwa mwanamuziki Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari, the Boss Lady.
Alipoulizwa kama ashawahi kuona meseji yoyote kwenye simu ya Diamond iliyowahi kumshtua, Zari alijibu kuwa katika makubaliano waliyowekeana tangu wanaanza mahusiano yao ya kimapenzi ni kuwa kila mmoja ashike simu yake. Pia alisema kuwa anajua kuna wadada lazima wanajirahisisha kwa mpenzi wake kwahiyo kuanza kushika simu yake ni kujitafutia ‘stress’ ambazo hazina ulazima wowote.

Zari aliulizwa pia kwamba jambo gani akilifanya linamkasirisha sana Diamond Platnumz ambapo alijibu kuwa watu wawili waliokulia kwenye mazingira tofauti wakiishi pamoja ni lazima kupishana kutakutokea, lakini Diamond hukasirishwa sana Zari anapompiga mtoto wao, Tiffah. Zari akitetea kitendo hicho amesema kuwa mtoto anapofanya makosa ni lazima anyooshwe, na kumchapa ni moja ya njia hizo za kumnyoosha.
Kuhusu swali hili, Diamond alijibu kuwa huwa anaumia moyo akiona watu wanamtongoza Zari na akasema kuwa kuna jamaa mmoja anakaa maeneo ya Mbezi Chini ana tabia ya kumtongoza mpenzi wake huyo. Lakini kwakuwa Zari anaishi nchini Afrika Kusini, anakuwa hapati tabu sana kuhusu hili.
Zari na Diamond kwa pamoja wamemuombea msanii Wema Sepetu amalize mapema matatizo yake polisi ili aweze kuhudhuria sherehe ya siku 40 tangu kuzaliwa kwa mtoto mwengine wa wawili hao, Prince Nillan. Wamesema kuwa hawana tatizo lolote na Wema Sepetu, hivyo wanaomba amalize matatizo kati yake na vyombo vya usalama ili aweze kuwepo kwenye shughuli hiyo itakayofanyika Jumamosi hii.
Zari alisema kuwa hana tatizo Wema kualikwa kwenye sherehe hiyo ya Maulid ya Prince Nillan, alipoulizwa kama atakubali Miss Tanzania huyo akitaka wawe marafiki alijibu kuwa hana tatizo na hilo kwani swala la yeye kuwahi kuwa katika mahusiano na Diamond ni suala lililotokea na lishapita.
Zari aliulizwa pia kuhusu ndoa, kwamba kama wana mipango yoyote ya kuhalilisha mapenzi yao hivi karibuni mipango ipoje. Jibu alilotoa ni kwamba hawajawahi kufikiria wala kuongelea kuhusu hilo lakini mwaka huu Diamond atakwenda kujitambulisha rasmi kwa baba wa Zari nchini Uganda. Alitoa sababu mbili za kutoipanga harusi hiyo kwa sasa kuwa kwanza wanataka harusi yao iwe kubwa zaidi kuwahi kutokea Afrika Mashariki kwahiyo wanahitaji muda wa kujiandaa kuifanya na pili ni kwamba kwa sasa wanawaza namna ya kuwaaandalia maisha bora watoto wao, kwahiyo wameamua kuwajengea ‘apartment’ zitazowasaidia kuwapatia pesa endapo itatokea bahati mbaya wao wasipokuwepo duniani.

from Blogger http://ift.tt/2kMeymZ
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment