Kamanda Sirro: Mbowe Jisalimishe Polisi; Masogange na Chid Mapenzi Tumewakuta na Madawa pia Wanatumia

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, limemtaka Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujisalimisha Polisi mara moja kwa ajili ya Mahojiano yanayohusu vita vya dawa za kulevya baada ya juhudi za kumsaka katika makazi yake kushindikana huku simu yake ya mkononi ikiwa imezimwa
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Simon Sirro amesema Bw. Mbowe aliahidi kwenda mwenyewe juzi tarehe 15, lakini hakwenda lakini jeshi la hilo lilimtafuta usiku na mchana katika makazi yake na kumpigia simu lakini simu yake ilizimwa
Aidha jeshi hilo limesema watuhumiwa watatu Agnes Masogange, Rashid Idd au Chid Mapenzi na Wallis Latif Nasher ambaye ni muuza magari katika eneo la mikocheni watapandishwa kizimbani Jumatatu kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya lakini pia walibainika wanaotumia dawa hizo baada ya kupelekwa kwa Mkemia Mkuu
Katika kupambana na Askari feki, jeshi limemtia mbaroni aliyekuwa askari Magereza wa cheo cha Koplo Peter Elias Msigwa aliyekuwa mtumishi katika gereza la keko, ambaye alifukuzwa kazi Desemba mwaka jana, lakini alikamatwa jana akiwa na mavazi ya kiaskari tena akiwa amejipandisha cheo kutoka koplo hadi Sajenti wa Polisi
Jeshi hilo pia limesema limewatia mbaroni watu 65 kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya pamoja na watuhumiwa 73 wa wizi na ujambazi wa kutumia silaha, mitambo mitano ya Gongo, lita 270 pamoja na Puli 250 za bangi.
Chanzo: Channel Ten

from Blogger http://ift.tt/2kAO9eV
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment