KWANINI TRUMP KALEGEZA MSIMAMO KWA CHINA

Siku ya Februari 10, dunia ilishangazwa kusikia yamefanyika mazungumzo kwa njia ya simu kati ya Marais Donald Trump wa Marekani na Xi Jinping wa Uchina.
Taarifa ya ikulu ya Marekani ilisema kuwa mazungumzo hayo yalikuwa “mazuri sana.” Na bila shaka yalikuwa muhimu zaidi kwa China kwa sababu Trump alimuhakikishia Xi kwamba Marekani inaunga mkono sera ya “China Moja.”
Mazungumzo haya ya simu, pamoja na barua binafsi kutoka kwa Trump kwenda kwa Rais wa China siku mbili kabla ya mazungumzo yao, ya kwamba Marekani ina lengo la kujenga “uhusiano wenye manufaa ” kati yake na China, iliondoa hali ya taharuki iliyokuwa imetengenezwa na Trump awali kwamba sera hii ya China inabidi izungumzwe tena na ikikumbukwa katika kampeni za kuwania urais mwishoni mwa mwaka jana, Trump aliahidi kwamba angepandisha kodi kwa bidhaa zinazoingia Marekani kutoka China kufikia asilimia 45, jambo lililoleta taharuki ya hali ya juu.
Ahadi hii iliwafanya viongozi wa mataifa mengi kumuunga mkono Trump, pengine kwakuwa walikuwa wanaichukia China au walitaka kupata nafasi ya kufanya biashara na Marekani, nafasi ambayo ingetengenezwa baada ya uhusiano kati ya Marekani na China kuharibika endapo ahadi ya Trump ingetimia. Lakini baada ya kuingia ikulu Trump amekumbana na upinzani mkali uliomfanya ashindwe kutekeleza ahadi hii na mwisho kukubali kuunga mkono sera za China na kuahidi ushirikiano kati ya nchi hizo. Sababu zilizoleta mabadiliko haya ni mbili:
Mivutano ya ndani
Baada ya kuingia ikulu, Trump amekutana na mambo ambayo awali hakuyategemea. Sera kadhaa alizopendekeza zimekumbana na upinzani mkali kutoka kwa wananchi, vyombo vya habari pamoja na mihimili mingine ya utawala.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kituo cha utangazaji cha CNN/ORC, idadi kubwa ya wananchi (asilimia 53), wanachukizwa na jinsi Trump anavyoendesha ofisi yake, hiki kikiwa ni kiwango kikubwa kabisa cha wananchi kumkataa Rais kuwahi kutokea kwa Rais mpya aliyeingia madarakani. Matokeo yake ni kwamba Trump amekuwa akitumia muda mwingi kujaribu kurekebisha uhusiano kati yake na wananchi.
Kwa kuzingatia hili, bila shaka miongoni mwa mambo ambayo Trump asingependa yatokee ni ugomvi kati ya Marekani na China, ugomvi utakaokuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea na wenye matokeo mabaya zaidi. Hii yaweza kuwa sababu kubwa ya kumfanya Trump afikirie upya juu ya sera za China kwa kulinganisha vipaumbele vya utekelezaji wa sera zake za ndani na nje ya nchi.
China yaishawishi ‘kichinichini’ familia ya Trump
Uamuzi wa Trump kulegeza msimamo wake kuhusu sera ya “China Moja” yawezekana pia ikawa ni matokeo ya mafanikio ya njia za diplomasia zilizotumiwa na China, wakiwa wametumia njia rasmi na zisizo rasmi.
Kupitia vyombo vya habari, China imekuwa imara na kutuma jumbe za mara kwa mara kwa Rais Trump kwamba sera ya “China Moja” ni ya msingi kwa China na kwamba watapambana mpaka mwisho kuona maslahi yake yanaheshimiwa na mataifa mengine, ikiwemo Marekani.
Pia, ikawa inatumia mlango wa nyuma kujaribu kumfikia Trump na kumfanya aelewe vizuri sera za mambo ya nje za nchi ya China.
Serikali ya jijini Beijing ilikuwa inatambua kwamba Trump kundi dogo sana la watu anaowaamini ambao ndio washauri wake anaowategemea sana, akiwemo mkwe wake, Jared Kushner na mtoto wake wa kike Ivanka Trump.
Kwa kujua hili, serikali ya Beijing imekuwa ikiwatumia hawa kuboresha uhusiano kati ya China na Rais Trump. Kulikoleza hili, mara tu baada ya Trump kushinda uchaguzi, Kushner alihudhuria chakula cha jioni kilichoandaliwa na bilionea wa Kichina, Wu Xiaohui, anayomiliki Shirika kubwa zaidi la bima nchini China, Anbang ambaye pia ana uhusiano wa karibu sana na watawala wa China.
Tarehe 1 Februari mwezi huu, mtoto wa kike wa Trump, Ivanka alifanya safari ya kushtukiza kwenye Ubalozi ya China uliopo jijini Washington, Marekani alipo hudhuria sherehe za mkesha wa mwaka mpya wa China.

from Blogger http://ift.tt/2lh2nPh
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment