LIONEL MESSI ANUNUA NYUMBA YA JIRANI YAKE, KISA WALIKUWA WANAPIGA KELELE

Lionel Messi amepata amelipatia tiba tatizo la majirani zake waliokuwa wanapiga kelele nyingi – kwa kuinunua nyumba waliyokuwa wanaishi na kuwafanya waondoke kabisa kwenye mtaa huo, amesema mchezaji mwenzake wa Barcelona Ivan Rakitic.
Messi mwenye umri wa 29, anaishi kwenye eneo la kifahari la Castelldefels jijini Barcelona pamoja na familia yake, lakini aliamua kuinunua nyumba hiyo ya jirani zake baada ya kuona wanamsumbua sana kwa kelele zao.
Tetesi za mshambuliaji huyu wa timu ya Taifa ya Argentina kununua nyumba ya jirani zake ilitolewa kwenye vyombo vya habari nchini Hispania miaka minne iliyopita – lakini sasa mchezaji mwenzake, Rakitic amethibitisha jambo hilo kwa kusema kwa Messi alifanya jambo hilo kwa sababu nyingi lakini mojawapo ikiwa ni kelele za majirani wake hao.

Ivan Rakitic anadai kwamba Lionel Messi alinunua nyumba ya jirani zake kuondoa tatizo la kelele
Messi na mkewe Antonella Roccuzzo wakiwa na watoto wao Thiago (4), na Mateo (1)

“Aliponunua nyumba yake iliyopo Castelldefels alikuwa analalamika kuwa jirani zake walikuwa wana kelele sana,” alisema Rakitic
‘Leo ilimlazimu kuinunua nyumba yao ili abaki peke yake na familia yake. Kwa bahati nzuri sijawahi kupata tatizo hilo.’
Jarida la Diariogol limeripoti kuwa majirani wa mcheza soka huyo walikuwa wakipangisha baadhi ya vyumba vya nyumba yao kitu kilichokuwa kinasababisha kelele za mara kwa mara kutoka kwa wapangaji wapya waliokuwa wanapiga muziki kwa sauti ya juu na kumsababishia kero Messi.

from Blogger http://ift.tt/2kM3juA
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment