MAKALA: KIPEPERUSHI CHANGU CHA DAWA ZA KULEVYA KIMFIKIE RAIS MAGUFULI

Rais wangu mpendwa, Dkt. John Magufuli. Nimevutwa kuzungumza nawe kuhusu dawa za kulevya, hii ni vita ambayo umeitolea mkazo kuwa kila anayehusika akamatwe, ikiwezekana hata mkeo, mama yetu mpendwa, Janet Magufuli.
Kweli kabisa hata mwandani wako akamatwe kama anahusika? Mama wa watoto wako unaowapenda? Hakika Rais wangu unachukia sana dawa za kulevya. Hii imekuwa alama yako kuwa wewe ni mtu wa maneno yako.
Kipeperushi changu hiki nakileta kwako kuonesha hisia zangu jinsi ninavyokuunga mkono. Nina sababu za kiwango cha mwisho kabisa cha namba za kukuunga mkono katika vita hii. Sababu zote nilizonazo zinatafsiriwa na maneno manne tu; nachukia dawa za kulevya.
Binafsi naamini Taifa kwa jumla linaunga mkono vita hii. Hata wale ambao wanakosoa utaratibu unaotumika wa sasa ulioanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, nao wanaunga mkono.
Shida iliyopo ni kuwa njia zinazotumika hazioneshi matarajio ya kufanikiwa vita yenyewe. Watu wanakosoa kwa sababu wanatamani kuona Tanzania inapata ushindi wa vita hii ili kuokoa nguvu kazi ya vijana wetu.
Wanakosoa kwa sababu wanataka kuona hatua mahsusi zinachukuliwa. Hatua ambazo zinafanana na ukubwa wa tatizo. Hatua ambazo zinatambua kuwa vita hii ni kubwa na yenye kuhitaji mapambano ya sayansi ya kiwango cha juu.

from Blogger http://ift.tt/2ls7P0o
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment