Maneno ya Zitto Baada ya IPTL Kuamriwa Kulipa Dola Milioni 168.8

Kupitia ukurasa wake Facebook Zitto kabwe amendika maneno hayo hapo chini…
Mahakama Ina uwezo wa kurejea maamuzi yake kwa kuitisha upya kesi zilizoamuliwa. Mfano mzuri ni kesi kuhusu umiliki wa Kampuni ya Simu ya Tigo ambayo ipo mahakamani Sasa SUO MOTO. 
Ni hatua nzuri Mahakama kuchukua ili kuhakikisha kuna HAKI na pia kuzuia UTAPELI kwenye biashara na kuweka heshima kwenye uwekezaji.
Hivi hii Mahakama haioni suala la PAP kumiliki IPTL na kuchota mabilioni ya fedha zilizokuwa Benki Kuu na kuendelea kulipwa tshs 300m kila siku izalishe au isizalishe umeme ? Ushahidi wote ulionyesha utapeli wa Kimataifa uliofanywa na Harbinder Singh Seth lakini kivuli cha uamuzi wa Mahakama umefanya MATAPELI hawa kuendelea kunyonya fedha kutoka TANESCO. Huu mrija wa PAP/IPTL upo kinywani mwa The Chato Inc? Ama ni JIPU la Mgongoni?
MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara imeiamuru Kampuni ya Kufua Umeme IPTL kuilipa Benki ya Standard Chartered Hong Kong na Benki ya Standard Chartered Malaysia Dola za Marekani 168,800,063.87.
Uamuzi huo ulitolewa na mahakama hiyo baada ya kukubali kuisajili hukumu iliyotolewa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara Uingereza ikiitaka kampuni hiyo kulipa fedha hizo.
Jaji Baker Sehel alitoa uamuzi huo baada ya kuisajili hukumu hiyo hivi karibuni na kuamuru IPTL kulipa fedha hizo.
Alisema walalamikiwa wanaweza kuwasilisha maombi ndani ya siku 21 ya kutaka usajili huo uwekwe pambeni na taarifa ya kusajili hukumu iwasilishwe kwa walamikiwa ikionyesha haitatekelezwa mpaka zipite siku 21.
Novemba 16 mwaka jana, Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara Uingereza ilisikiliza kesi hiyo baada ya walalamikiwa kushindwa kuwasilisha utetezi wao.
Walalamikaji katika kesi hiyo walikuwa Standard Chartered Bank Hong Kong Limited na Standard Chartered Bank Malaysia wakati walalamikiwa ni IPTL, VIP Engeneering and Marketing Limited na Pan Africa Power Limited.
Katika shauri hilo walalamikiwa walishindwa kuwasilisha utetezi kwa madai kwamba mtambo wa IPTL na yote yanayohusu kampuni hiyo yako Tanzania na kwamba kabla ya kesi hiyo kuna kesi nyingine mbili nchini.
Inadaiwa msingi wa kesi hizo ni kuhusu uhalali wa Standard Chartered Bank kuwa mdai halalali wa IPTL.
Katika kesi moja, IPTL na PAP wanaidai Standard Chartered Bank Sh trilioni sita na ya pili, VIP wanaidai benki hiyo Sh trilioni moja.
Pamoja na kuwasilisha pingamizi, mahakama ilitupilia mbali na kusikiliza kesi hiyo upande mmoja.

from Blogger http://ift.tt/2luoWjy
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment