Wakati mapambano dhidi ya dawa za kulevya yakiendelea kushika kasi maeneo mbalimbali ya Tanzania, mambo mbalimbali yanayohusishwa na visa vya watu kukamatwa vimeendelea kuibuka kila iitwapo leo huku baadhi ya watu wakionyesha namna walivyotajwa katika orodha kwa chuki binafsi.
Awali kulikuwa na tuhuma kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo pia wabunge waliokuwa wakidai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hakumtaja mwanadada Agness Gerald Waya maarufu Masogange kwa sababu wawili hao wanauhusiano wa kimapenzi na kuwa RC Makonda amempangia mrembo huyo nyumba maeneo ya Mbezi.
Wakati hayo yakiendelea, na Masogange akiwa amekamatwa na kuachiwa kwa dhamana, kwenye mitandao ya kijamii zimesambaa sauti za majibizano ya kwenye simu zinazosemekana ni za Mama mzazi wa Wema Sepetu na Steven Nyerere wakizungumzia kukamatwa wa Wema.
Miongoni mwa mengi waliyoyazungumza ni jinsi Makonda alivyomdhalilisha Wema Sepetu, Makonda alivyowahi kumtongoza mwanadada huyo na mipango ya Chadema juu ya vita ya dawa za kulevya iliyoanzishwa na RC Makonda.
Aidha, katika maongezi hayo, wametajwa viongozi wengine kama Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlingwa (mtoto wa Celina Kombani).
Hapa chini ni sauti zinazodaiwa ni za Steven Nyerere na Mama Wema Sepetu wakizungumza kwa njia ya simu.
ANGALIA VIDEO CHIDEO
from Blogger http://ift.tt/2lzFpmC
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment