Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) Tawi la Dar es Salaam wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala wakituhumiwa kuchapisha picha kupitia mtandao wa WhatsApp za kumkashifu Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Wanafunzi hao ambao ni Amenitha Kongo (19), Maria Tweve (20), Agnes Gabriel (21) na Anne Mwansasu (21) walipandishwa kizimbani jana wakiwa chini ya ulinzi wa askari ambapo walisomewa shtaka la kuchapishwa picha za kumkashifu Rais Dkt Magufuli mbele ya Hakimu Mkazi, Catherine Kiyoja kitendo ambacho ni kinyume na Sheria ya Makosa ya Mitandao ya mwaka 2015.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kuchapisha picha ambazo zinamuonyesha Rais Dkt Magufuli akiwa amevalia hijab kama mwanamke wa Kiislamu na kisha kuzisambaza kitendo ambacho walijua kabisa ni kinyume na sheria.
Watuhumia wote walirejeshwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Hii si mara ya kwanza kwa watu mbalimbali kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumkashifu Rais Magufuli au viongozi wengine wa serikali.
Katika kesi ya hivi karibuni, mtunza bustani katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam, Maganga Masele (25) alipandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shtaka la kumtukana Rais Dkt Magufuli na Makamu wa Rais Samia Suluhu.
ANGALIA VIDEO CHIDEO
from Blogger http://ift.tt/2mblQRh
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment