Wafanyakazi katika afisi ya Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe walimuandalia karamu ya kukata na shoka kusherehekea kiongozi huyo kutimiza miaka 93 jana Jumanne.Kulikuwa na keki kubwa.
Bw Mugabe ndiye kiongozi wa nchi mwenye umri mkubwa zaidi duniani.
Kutakuwa na sherehe kubwa kwa ajili ya umma Jumamosi.
Rais Mugabe aliongoza Zimbabwe kupata uhuru wake mwaka 1980 na ametangaza kwamba anapanga kuwania katika uchaguzi mkuu mwaka ujao, ambapo atakuwa na umri wa miaka 94.
Mugabe alizaliwa 21 Februari, 1924.
Alifungwa jela 1964-1974 kwa kutoa “hotuba ya kuhujumu serikali”
Baada ya kuachiliwa, alisaidia kuongoza vita dhidi ya serikali ya Rhodesia
Vita vilipomalizika, Mugabe alishinda uchaguzi 1980 na akawa waziri mkuu wa Zimbabwe na akaongoza taifa hilo kama waziri mkuu hadi mwaka 1987.
Alipokuwa anasherehekea kutimiza miaka 93, Umoja wa Ulaya ulipiga kura kuongeza vikwazo dhidi yake.
Katika sherehe hiyo ya Jumanne, Bw Mugabe alisaidiwa kukata keki na mkwewe Simba Chikore.Mugabe akikata keki
Bw Mugabe pia alipewa zawadi mbalimbali, zikiwemo kiti hiki, kwa kutimiza miaka 93. Kulikuwa pia na saa na kalamu.
Akihutubu wakati wa sherehe hiyo, Bw Mugabe alimshukuru Mungu kwa kumjalia maisha marefu.
Alionekana kufurahia kula keki.
-bbcswahili
ANGALIA VIDEO CHIDEO
from Blogger http://ift.tt/2l7pLxF
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment