WASIFU WA MUIGIZAJI WEMA SEPETU

Jina lake kamili ni Wema Isaack Abraham Sepetu. Amezaliwa katika familia ya kibalozi ambapo baba yake ni Balozi Isaack Abraham Sepetu.
Wema Sepetu kama anavyofahamika zaidi alizaliwa Septemba 28, 1988 katika Hospitali ya Dr. Andrew (Dr. Andrew’s Hospital) akiwa ni mtoto wa nne katika familia ya Mzee Isaack yenye watoto wanne wote wakiwa ni wakike.
Balozi Isaack Abraham Sepetu.
Alipata elimu yake ya msingi na sekondari katika shule ya Academy International School iliyopo jijini Dar es Salaam, Tanzania ambapo baada ya kuhitimu alijiunga na chuo, Limkokwing University of Creative Technology cha nchini Malaysia ili kusomea masuala ya biashara za kimataifa ambapo alisoma kwa mwaka mmoja baadae aliacha na kuendelea na uigizaji.
Wema Sepetu au Sepenga kama watu wanavyomuita kwa utani, alianza kuigiza tangu akiwa shule ya msingi ambapo alishiriki shughuli mbalimbali za sanaa akiwa Dar es Salaam. Lakini aliingizwa rasmi kwenye tasnia ya filamu nchini Tanzania na aliyekuwa mpenzi wake, marehemu Steven Kanumba kipindi wakiwa na uhusiano.
Wema alitokea kwa mara ya kwanza katika filamu ya Point of No Return akiwa na Steven Kanumba, na tangia hapo ameshiriki katika filamu nyingine nyingi ikiwa ni pamoja na Family Tears, Red Valentine,White Maria. Kote alifanya vizuri na kumfanya kuwa msanii wa kike anayevutia zaidi.
Wema Sepetu akiwa na aliyekuwa mpenzi wake, marehemu Steven Kanumba.
Kuhusu masuala ya urembo, wengi watakubaliana kuwa Wema Sepetu ni miongoni mwa wasichana warembo nchini Tanzania. Mwaka 2006 alishinda taji la Mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania) shindalo lililofanyikia katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Zaidi ya wasichana 20 kutoka mikao 25 ya Tanzania walikuwa wakiwania taji hilo.
Miss Tanzania 2006, Wema Isaack Sepetu.
Baada ya kutwaa taji hilo Wema Sepetu alizawadiwa gari aina ya Rav 4 na kuwa amejikatika tiketi ya kushiriki shindano la kumsaka mrembo wa Dunia (Miss World). Wema alisafiri kwenda Warsaw nchini Poland kwenye shindano hilo lakini hakufanikiwa kutwaa taji badala yake lilikwenda kwa Taťána Kuchařová kutoka Jamhuri ya Czech.
Licha ya kuwa muigizaji lakini pia ni mjasiriamali, anamiliki kampuni ya filamu ya Endless Fame Film lakini pia anakipaji cha utangazaji.
Aidha, Sepetu amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mwanamuziki Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz lakini pia mshindi wa taji la Big Brother Afrika 2014, Idris Sultan.
Wema Spetu na Diamond Platnumz
Kwa sasa Wema Sepetu anakabiliwa na kesi ya dawa za kulevya ambapo inadaiwa kuwa msokoto mmoja wa bangi na karatasi za kuvutia bangi (rizla) vilikuwa nyumbani kwake.
Wema Sepetu hajaolewa na wala hana mtoto.

from Blogger http://ift.tt/2l6bWlH
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment