WAZIRI HARRISON MWAKYEMBE AANDIKIWA BARUA YA ONYO

Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS) kimemwandikia barua Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kikimtaka aache kuingilia uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS). Barua hiyo imekuja baada ya Dkt. Mwakyembe kudaiwa hivi karibuni kutishia kuifuta TLS kwa madai kwamba imeanza kuingiliwa kisiasa.
Barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na Rais wa EALS, Richard Mugisha, inasema TLS si chama cha kisiasa na kimeanzishwa kwa kufuata sheria zote. “Mheshimiwa Waziri, tumesikitishwa na taarifa ambazo zimeenea kwenye vyombo vyote vya habari na gazeti la East African la Februari 18 ambalo limekunukuu ukisema kwamba Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kina muingiliano wa kisiasa,” inasema sehemu ya barua hiyo.
Katika barua hiyo, Mugisha anasema wanasheria wanatakiwa wapewe uhuru, wasiingiliwe na serikali kama ilivyo kwa nchi nyingine kwani kuingilia ni sawa na kuvunja sheria za nchi.
Rais wa sasa wa TLS, John Seka amesema kuwa chama chake kimefurahishwa na barua hiyo kwa Waziri na kwamba nao pia wanafanya taratibu kumuona ili kujadili mustakabali wa chama hicho. Alisema kuwa TLS inaendelea na mchakato wa uchaguzi kama ulivyopangwa na kuwataka wagombea wote kujiandaa kwa uchaguzi huo ambao alisema ni halali.
Uchaguzi wa chama hicho unatarajiwa kufanyika machi 18 mwaka huu, huku wagombea kutoka vyama vya upinzani wakiwa wamejitokeza kuwania nafasi ya uongozi wa juu.

from Blogger http://ift.tt/2meZr8X
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment