Watu 12 wamejeruhiwa na watatu kati yao
wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa baada ya kutokea ajali
iliyohusisha magari mawili ya abiria na lori moja, katika eneo la Mlima wa
Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Akizungumza baada ya kutokea kwa ajali
hiyo , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi alisema magari
yote matatu yaliyohusika kwenye ajali hiyo yalikuwa yakienda jijini Dar es
Salaam.
Ameyataja mabasi yaliyohusika kwenye ajali
hiyo kuwa ni ya Kampuni ya Happy Nations, Abood na gari moja la mzigo.
Mjengi amesema katika ajali hiyo watu 12
walipata majeraha na watatu kati yao wamefikishwa Hospitali ya Rufaa ya mkoani
Iringa kwa matibabu na tisa kati yao walitibiwa na kuruhusiwa kutoka hospitali.
Kamanda huyo ametaja chanzo cha ajali kuwa ni
dereva wa gari la Abood lililokuwa nyuma ambaye aliligonga basi la Happy
nations ambalo nalo liligonga gari lilikuwa mbele yake na kusababisha magari
yote kuserereka na kutoka pembeni mwa barabara.
0 maoni:
Post a Comment