Jeshi la Polisi nchini linamshikilia Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu.
Lissu aliachiwa leo asubuhi na Hakimu Mkuu
Mkazi, Huruma Shahidi baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Paul
Kadushi kuwasilisha hati ya kuondoa shtaka hilo.
Kadushi aliwasilisha hati hiyo chini ya
kifungu namba91 (1) cha makosa ya jinai akionyesha DPP hana haja ya kuendelea
na kesi, mahakama ikaridhia na kumuachia.
Muda mfupi baada ya kuachiwa na kutoka nje ya
mahakama alikamatwa tena na askari waliokuwapo mahakamani hapo na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi.
Lissu alikuwa anashtakiwa kwamba Januari 11,
mwaka huu katika kampeni za uchaguzi jimbo la Dimani aliwashawishi watu
wasiridhike na wawe na nia ovu dhidi ya utawala.
0 maoni:
Post a Comment