Msanii wa bongo movie Shamsa
Ford amesema watanzania waache kuropoka na kuongea bila kujua
kinachoendelea kuhusu yeye na msanii mwenzake Gabo.
Akiongea
kupitia kipindi cha eNewz, Shamsa amesema hata mume wake anaelewa
kinachoendelea na hana wasiwasi na Gabo, huku akiwashukuru watu
wanaosambaza taarifa hizo kwa kumsaidia kutangaza movie
"Tuache mambo ya kukurupuka
kuongea kwamba nimejiweka kwa Gabo wakati hawajui kitu gani kinaendelea
baina yetu ila nashukuru kwa kuwa wametusaidia kutangaza movie yetu
kwani hata mume wangu mwenyewe anacheka tu" amesema Shamsa.
Shamsa amelazimika kutoa ufafanuzi baada
ya hivi karibuni kupost picha akiwa na Gabo, na kumtaja msanii huyo
kuwa ndiye ambaye humkosha katika uigizaji, na kwamba akiwa anaigiza
naye, huhisi kama anafanya kweli.
Hata hivyo Shamsa hakusita kuongelea
suala na mume wake kutajwa katika tuhuma za madawa ya kulevya na kusema
kuwa kabla ya kuolewa aliambiwa atapitia mambo mengi matatizo, shida,
raha na changamoto nyingi sana katika ndoa lakini anashukuru Mungu kwa
kila kitu.
"Hiki ni kipidi ambacho nimekuwa karibu na mume wangu kuliko siku zote tunavyokuwa karibu" Alimalizia Shamsa.
Shamsa na mumewe, Chid Mapenzi
0 maoni:
Post a Comment