Mchezaji tennis namba 1 katika viwango vya ubora Duniani Andy Murray, amefanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya mashindano ya wazi ya tennis ya Barcelona baada ya kumshinda Albert Ramos-Vinolas.Murray amelipa kisasi katika ushindi huo baada ya mchezaji huyo Ramos-Vinolas kumtoa katika hatua ya nne ya mashindano ya Monte Carlo.
Mschezaji huyo kutoka Scotland, amepata ushindi wa seti 2-6 6-4 7-6 (7-4) katika mchezo huo uliodumu kwa takribani masaa mawili na dakika 59. Murray kwa sasa atakabiliwa na Mchezaji Dominic Thiem kutoka nchini Australia kwa mchezo wa hatua ya Nusu Fainali.
Ramos-Vinolas, ambaye anashikilia nafasi ya 19 katika viwango vya ubora vya mchezo huo duniani, alifanikiwa kucheza vizuri zaidi katika seti ya kwanza ya mchezo huo, kabla mambo kugeuka katika seti ya pili ambayo Murray aliweza kufanya vizuri zaidi.
Katika Pambano hilo huko Barcelona, Mhispania huyo aliweza kupata majeraha katika mchezo huo, tukio ambalo Mchezaji Ramos-Vinolas alinufaika nalo kabla Mchezo kubadilika kwa Murray kujitibu na kuwa mgumu kwa upande wa Ramos-Vinolas.
BY HAMZA FUMO
0 maoni:
Post a Comment