Italy hajulikani Alikiba wala Diamond – Hussein Machozi







Msanii wa muziki, Hussein Machozi, amefunguka kwa kudai kuwa, hakuna msanii wa muziki kutoka Tanzania ambaye anajulikana nchini Italy.

Aidha amedai muimbaji kutoka Kenya, Stella Mwangi ambaye anaishi nchini Norway, ndiye msanii wa Afrika Mashariki anayefanya vizuri nchini humo.

Muimbaji huyo aliyewasili nchini Tanzania wiki hii akitokea Italy, amedai muziki wa Tanzania haujafika huko na hata wasanii wanaofanya vizuri nchini kwa sasa akiwemo Diamond na Alikiba hawajulikani.
“Hapana lakini kuna mtu mmoja alishaniambia kuhusu msanii wa Kenya anaitwa Stella Mwangi wanamfahamu fahamu, siyo kivile sana kutoka East Africa,” alisema Hussein.
Aliongeza, “Bongo Fleva Italy sijawahi kuisikia kiukweli wa Mungu. Kama kuna mshikaji mmoja nilimwambia kwetu kuna msanii mkali sana anaitwa Diamond nikawa nimempa link akawa shabiki, akawapa na wengine wakawa mashabiki wa Diamond kinyama.,”
Muimbaji huyo amedai amekuja nchini kwaajili ya kuachia kazi zake mpya za muziki na baada ya hapo atarejea tena Italy kwaajili ya kuendelea na masomo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment