Fahamu: Taarifa kuhusu homa ya majano






Ugonjwa wa homa ya manjano kitaalamu huitwa “HEPATITIS”. Ugonjwa huu ni hatari sana,na unasababishwa na virus aina ya Hepatitis.Virusi hivi mara nyingi hushambulia eneo la ini kwenye mwili wa binadamu.

Ugonjwa huu usipotibiwa mapema husababisha uvimbe katika ini na hatimaye husababisha saratani. Mara nyingi ugonjwa huu haujionyeshi moja kwa moja.
Baadhi ya dalili za ugonjwa huu ni pamoja na:
Baadhi ya vielekezi vya homa hiyo mwilini huwa ni, mwili kuwa dhaifu,kujisikia kichefu chefe,homa kali kupita kiasi, maumivu makali ya tumbo upande wa ini, macho na ngozi kuwa ya njano, mkojo kuwa na hali ya uweusi na unakuwa mzito n.k.

Hizi ndio njia utakazoweza kuzuia maambukizi kwa watu wengine.
Nyumbani:
1.Usishirikiane kutumia nyembe, miswaki au visu vya kucha;
2.Safisha kwa uangalifu damu yoyote kwa kutumia mifuko ya mkono ya mpira, sabuni, maji moto na dawa ya kuua wadudu;
3.Weka vitu vyovyote vinavyokuwa na damu, kwa mfano plasta, bandage, tampon kwenye mfuko wa plastiki ndipo uziwekee kwenye pipa la taka;
4.Epuka matendo mengine ya kujamiiana yanayosababisha kugusa damu-kwa-damu, kwa mfano kujamiiana wakati wa hedhi

Maambukizi ya virusi vingine.
Maambukizi ya virusi vingine maana yake ni ambukizo la virusi zaidi ya kimoja. Watu wenye homa ya manjano wanaweza kuambukizwa VVU na/au homa ya manjano B, kwa sababu huenezwa kwa njia zilezile za kugusisha damu-kwa-damu. Maambukizo yanaweza kuharakisha maendeleo ya homa ya manjano na kuzidisha hatari ya kupata ugonjwa au kansa ya ini.
Njia za kudumisha afya na kupunguza hatari ya ugonjwa wa homa ya majano.

Endelea kula chakula bora chenye mafuta, sukari na chumvi kidogo
Punguza au acha kunywa pombe
Pumzika vizuri
Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara
Jaribu kuepuka au kutawala msongo
Kunywa maji mengi
Epuka kutumia dawa zinazoweza kusababisha madhara zaidi ya ini lako
Ukiamua kutumia vitamini au dawa nyingine (k.m. mitishamba) zungumza na daktari au muuguzi wako.

Mnamo mwaka jana Hospitali ya Taifa Muhimbili, ilitarajia kufanya uchunguzi wa virusi vya homa (hepatitis B) na kutoa tiba kwa kutumia dawa ya Tenofovir.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Matumbo, John Rwegasha amesema ugonjwa wa homa ya ini ni hatari na kwamba maambukizi yake yanashabihiana na yale ya virusi vya ukimwi.
Na Laila Sued
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment