Shirikisho la Soka Duniani, (FIFA) limetoa orodha ya viwango vya soka kwa wanaume duniani vya mwezi huu,ambapo kwa mujibu wa orodha hiyo, Tanzania imeendelea kushikilia nafasi ya 135 kama ilivyokuwa mwezi uliopita.
Mwezi uliopita Tanzania Ilipanda kwa nafasi 26 kufuatia kushinda mechi mbili mfululizo dhidi ya Botswana na Burundi.
Kwa ukanda wa Afrika Mashariki, Uganda wameendelea kuongoza kwa kukamata nafasi ya 72,wakifuatiwa na Kenya ( 78 ) kwenye viwango vya Duniua.
Kwa upande wa nafasi 50 za timu za juu kwenye viwango vya FIFA, hakuna mabadiliko yoyote kwani Brazil wameendelea kuongoza mbele ya Argentina na Ujerumani huku Senegal katika nafasi ya 30 wakiongoza barani Afrika.
By Godfrey Mgallah
0 maoni:
Post a Comment