Prezzo amtishia maisha msanii Kaka Sungura
Unyamavu wa staa na rapper mkongwe hapa nchini Kenya kwenye muziki maarufu kama Prezzo, haujawa pingamizi kwake kutoziteka headline za vyombo vya habari.
PrezzoWiki iliyopita Prezzo amekuwa akirusha cheche kali za vitisho kwa maaadui wake haswa wale ambao wameonekana wakimnyemelea x-wake kwajina Michele Yola. Prezzo amedai kuwa Michele bado ni wake mpaka atakapo muona ameolewa. Kwahivyo hakuna rukhusa ya mtu yeyote kupiga picha au video naye bila idhini yake.
Wakati vurugu zake kwenye mitandao ikiendelea, Prezzo ameonekana mwenye jazba , na hatimaye imebainika ni nani ambaye alikuwa anamlenga. Japo hakuna ushaihidi wowote kama mtu ambaye ametishiwa maisha amewahi kuonekana kumkejeli ama kumchokoza Prezzo, Prezzo ameamua kufichua kinacho muumiza moyoni mwake. Kupitia ukurasa wake instagram, alipost picha ya mwanadada ambaye anaonekana ameinama tayari akiwa mkononi ameshika bunduki ili kulenga shabaha.
Kaka SunguraNa chini yake kuandika caption iliyolenga moja kwa moja kwa Rapper na muasisi wa kampuni ya muziki nchini Kenya Kaka Sungura Empire maarufu kama King Kaka. Haya ndio maneno aliyoyaandika Prezzo kwenye instagram. ”prezzo254Kaka sunguch best watch his mouth my cousin sista finna take care of u #Rapcellency #TulyUnruly”
Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram:changez_ndzai
0 maoni:
Post a Comment