Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amesema Serikali haina mpango wa kusitisha mbio za Mwenge wa Uhuru.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama
Waziri Muhagama amelisema hilo Bungeni leo, Mjini Dodoma baada ya Mbunge mbunge wa Konde, Khatib Said Haji kuhoji,
Je? Bado kuna faida kwa watanzania kuendelea kukimbiza Mwenge wa Uhuru kila mwaka? Kama zipo ni faida gani? Kama hakuna faida,Je? Ni lini Mwenge huu utasitishwa?“Faida za Mwenge wa Uhuru Kitaifa na Kimataifa ni pamoja na kuhamasisha hali ya wananchi kujitegemea na kuwekeza katika maeneo mbalimbali katika taifa letu, pia ni chombo pekee cha kujenga mshikamano na kudumisha amani, pale ambapo Mwenge unapita na bila kujihusisha na itikadi za kisiasa, kuendelea kuhamasisha umuhimu wa Muungano kwa Watanzania wa nchi mbili wa nchi yetu, na kila mwaka kufungua kuweka maeneo ya msingi kama miradi mbalimbali ya wananchi, na kuhamasisha uzalendo na kuendelea kujitolea,” amesema Waziri Muhagama.
“Mwenge wa uhuru umeendelea kumulika hata nje ya mipaka yetu , umoja na mshikamao wa Watanzania ni matunda pia ya Mwenge wa Uhuru kwahiyo kutokana na mafanikio na faida zilizopatikana kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru Serikali inatambua kuwa zipo faida za kuendelea kukimbiza Mwenge huu wa uhuru, Hivyo basi Serikali haina mpango wowote wa kusitisha mbio za Mwenge wa Uhuru kwahiyo litakuwa ni endelevu na litaendelezwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine kwa kusisitiza misingi hii bila kuchoka.”
0 maoni:
Post a Comment