TFF yajitosa kupinga ujangili wa wanyama pori








Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi leo amesaini mkataba wa ushirikiano na taasisi ya Wild Aid Tanzania inayojihusisha na vita dhidi ya ujangili wa wanyama pori.
Katika shughuli hiyo fupi, Malinzi alisema ushirikiano huo utaanza kufanyiwa kazi kupitia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.

“Kama mnavyofahamu, shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ina majukumu makubwa matatu, kuendeleza, kupromote na kuongoza mchezo kwa mujibu wa sharia, lakini upande wa jamii huwa pia tunapenda kujihusisha na mambo mbalimbali,”amesema.
Malinzi amesema huo ni mwendelezo wa mahusiano mazuri kati ya TFF na Jamii huku akisema Wild Aid itautumia mpira wa miguu kikamilifu katika kampeni zake za kutunza wanyama pori.

Kwa upande wake, Ofisa wa Wild Aid Tanzania, Lilly Massa amesema kwamba, wamefurahi kuingia kwenye mahusiano na TFF na mpira wa miguu Tanzania kwa ujumla.
Alisema tayari wapo na mahusiano na mchezaji nyota wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet anayecheza Marekani na mwanamuziki Ali Kiba hivyo kuongezeka kwa TFF ni hatua nyingine nzuri kwao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment