Msanii Roberto kutoka Zambia amemtaja msanii wa Bongo Fleva, ambaye atasikika kwenye albamu yake mpya.
Muimbaji huyo ambaye amewahi kufanya vizuri kupitia wimbo wake wa Amarula, amemtaja msanii huyo kuwa ni Vanessa Mdee.
“Kuna nyimbo 12 kwenye albamu yangu mpya, pamoja na nyimbo mbili za ziada, hivyo jumla ni 14. Nimewashirikisha wasanii kama Patoranking (Nigeria), Vanessa Mdee (Tanzania), Dammy Krane (Nigeria), Jay Rox (Zambia), kundi la BrathaHood, General Ozzy, Mandela na Young Rico,” amesema Roberto kupitia kipindi cha Mtaa wa Pili cha Choice FM.
Msanii huyo ameongeza kuwa albamu hiyo itaitwa ‘Super Star’ na itatoka Mei 25 mwaka huu.
0 maoni:
Post a Comment