Ajax kuvaana na Man United fainali ya UEFA Europa League

 

 

 
 
Baada ya usiku wa May 10 kufahamu fainali ya UEFA Champions League itazikutanisha timu gani, jana usiku ilichezwa michezo ya marudiano ya nusu fainali ya UEFA Europa League, Man United wakicheza dhidi ya Celta Vigo na Lyon wakicheza dhidi ya Ajax.

Mechi ya Man United ilimalizika kwa sare ya kufungana 1-1 goli la Man United likifungwa na Fellaini dakika ya 17 na goli la Celta Vigo likifungwa dakika ya 85 na Roncaglio, sare hiyo imeiwezesha Man United kuingia hatua ya fainali baada ya mchezo wa kwanza kuifunga Celta Vigo goli 1-0 ugenini. Ajax wao wamepoteza kwa magoli 3-1 lakini wamefuzu kuingia fainali kwa jumla ya mabao ambayo ni 4-5, Man United inafuzu kucheza fainali ya Europa League kwa mara ya kwanza wakati Ajax inafuzu kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21 mara ya mwisho ilikuwa 1996. Mchezo wa fainali ya UEFA Europa League utachezwa katika uwanja wa Friends mjini Stockholm nchini Sweden May 23 2017, hii inakuwa ni mara ya pili kwa kocha wa Man United Jose Mourinho kufanikiwa kufikia hatua ya fainali ya michuano hiyo akiwa na timu mpya katika msimu wa kwanza, mara ya kwanza ilikuwa 2002/03 akiwa na FC Porto ya kwao Ureno.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment