Korea
Kaskazini imesema kuwa itafanya mazungumzo na Marekani iwapo mazigira
yataruhusu ,kulingana na vyombo vya habari vya Korea Kusini.
Mjumbe mwandamizi wa Korea Kaskazini amesema kuwa mazungumzo na
serikali ya rais Trump yanawezekana kufuatia mkutano na waliokuwa
maafisa wa serikali ya Marekani nchini Norway.
Awali mwezi huu rais wa Marekani Donald Trump alisema itakuwa heshima kubwa kukutana na rais Kim Jong un.
Matamshi yake yanajiri kufuatia ongezeko la hali ya wasiwasi kuhusu
mipango ya Korea Kaskazini ya kinyuklia pamoja na ile ya utengezaji wa
makombora ya masafa marefu.
Choe Son Hui ambaye ni afisa katika wizara ya maswala ya kigeni
kuhusu maswala ya Marekani kaskazini alitoa matamshi hayo wakati
alipokuwa akirudi Pyongyang baada ya mkutano mjini Oslo.
0 maoni:
Post a Comment