Bosco Ntaganda, akiwa ndani ya Mahakama ya ICCREUTERS/Toussaint Kluiters/United Photos/Pool
Aliyekuwa
kiongozi wa kundi la waasi la FPLC nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo Bosco Ntaganda, hatimaye atatoa ushahidi wa kujitetea katika
Mahakama ya Kimataifa ya ICC siku ya Jumatano.
Ntaganda
maarufu kama "The Terminator" amekuwa akikanusha madai kuwa aliwatumia
watoto wadogo kama wapiganaji na kuwatumia wanawake na wasichana kama
watumwa wa kingono.
Kesi dhidi ya Ntanganda ilianza miaka miwili iliyopita mjini Hague, alipofunguliwa mashtaka ya mauaji katika jimbo la Ituri yaliyotokea kati ya mwaka 2002 na 2003.
Ntaganda mwenye umri wa miaka 43, amekanusha madai yote 13 ya uhalifu wa kivita na mengine matano ya ukiukwaji wa haki za binadamu, yaliyotekelezwa na waasi hao.
Watu zaidi ya 60,000 walipoteza maisha na wengine kuyakimbia makwao baada ya kuvamiwa na waasi hao.
Kabla ya kufikishwa katika Mahakama ya ICC, Ntaganda alijisalimisha katika Ubalozi wa Marekani jijini Kigali nchini Rwanda mwaka 2013.

0 maoni:
Post a Comment