Magaidi wa Al Shabab wazuiwa kuingia nchini Kenya


mediaMagaidi wa Al Shabab nchini Somalia
Polisi nchini Kenya wamefanikiwa kuwazuia magaidi sita wa Al Shabab kutoka nchini Somalia, waliokuwa wanapanga kuingia nchini humo kwa lengo la kutekeleza shambulizi la kigaidi.
Inspekta Mkuu wa Polisi nchini humo Joseph Boinnet amesema washukiwa hao, wawili raia wa Kenya na wengine kutoka Somalia, walikuwa wametumwa na Kamanda wao kutoka kambi yao ya Burhanche.
Boinett amesema, maafisa wa usalama nchini Kenya walifanikiwa kuzuia shambulizi hilo kwa sababu ya ushirikiano wa karibu na wenzao wa Somalia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mafanikio haya ya jeshi la Polisi nchini humo limekuja baada ya maafisa 20 wa Polisi kuuawa wiki kadhaa zilizopita Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya magari waliyokuwa wanasafiria kukanyaga mabomu yaliyotegwa ardhini.
Kenya imeendelea kutishiwa usalama na kundi la Al Shabab baada ya kutuma wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na kundi hilo mwaka 2011.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment