Kambi ya Ngomoromo katika Wilaya ya Lamwo Kaskazini mwa Uganda, inayowapa hifadhi wakimbizi kutoka Sudan Kusini
Marais
na wawakilishi wa serikali kutoka Mataifa ya Afrika Mashariki katika
muungano wa IGAD, wanakutana jijin Addis Ababa nchini Ethiopia
kujadili hali ya usalama na wakimbizi nchini Sudan Kusini.
Waziri
Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ambaye pia ni Mwenyekiti wa IGAD
anaongoza mkutano huo kujaribu kutafuta suluhu ya kuwasaidia maelfu ya
raia wa nchi hiyo wanaoteseka lakini pia kumaliza vita nchini humo.
Hata hivyo, rais Salva Kiir alikataa mwaliko wa kushiriki katika mkutano huo na kumtuma Makamu wake Taban Deng Gai.
Ikulu ya Juba imeripoti kuwa rais Kiir ana majukumu mengine muhimu yanayomfanya kutohudhuria mkutano huu.
Mashirika ya kutetea haki za Binadamu na asasi zingine za kiraia kama Enough Project, yanatoa wito kwa IGAD kuanza kufikiria mbinu mpya ya kumaliza vita vinavyoendelea.
Mkurugenzi Mkuu wa asasi hiyo Jon Temin, amesema kuwa mkutamo huu ni muhimu sana na unatoa nafasi kwa IGAD na Jumuiya ya Kimataifa kumaliza kabisa mzozo wa Sudan Kusini.
Mkataba wa amani kati ya rais Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar uliotiwa saini mwaka 2015, ulivunjika na kusababisha kuendelea kwa vita vinavyoendelea hadi sasa.
Rais Kiir mwezi uliopita alizundia mazungumzo ya kitaifa nchini humo na kutangaza kumalizika kwa vita, hata hivyo mapigano yameendelea kushuhudiwa nchini humo.

0 maoni:
Post a Comment