Maandamano katika mji wa Caracas Jumapili Julai 30, 2017, wakati wa kura.
Uchaguzi
wa bunge la Katiba ulifanyika siku ya Jumapili nchini Venezuela,
uchaguzi ambao uliitishwa na rais Nicolas Maduro. Baada ya kupiga kura,
watu 537 watachaguliwa kwenye Bunge Maalum. Bunge hili litakua na
mamlaka ya "kuandika katiba mpya."
Wapiga
kura milioni 20 walitakiwa kushiriki uchaguzi huo ambao upinzani
ulisusia. Zoezi hilo liligomewa na vyama vya upinzani vinavyompinga Rais
Nicolas Maduro vyenye wabunge wengi katika bunge la Venezuela..
Upinzani unaona kwamba hiyo ni mbinu ya serikali ya kutaka kusalia
madarakani."
Uchaguzi huu ulifanyika katika hali ya vurugu. Mgombea mmoja alipigwa risasi nyumbani kwake katika mji wa Ciudad Bolivar usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili na asubuhi, kiongozi wa upinzani aliuawa katika maandamano dhidi ya Bunge la Katiba katika mji wa Cumana. Katika mji mkuu wa Venezuela, Caracas, askari wasiopungua wanne walijeruhiwa katika mlipuko. Kwa jumla, watu wasiopungua kumi waliuawa katika siku inayotajwa kuwa ni umwagikaji damu baada ya miezi minne ya machafuko.
Matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa licha ya maandamano makubwa yanayoendeshwa na upinzani.
Kumekuwa na mapambano kati ya polisi na waandamanaji ambao wanapinga Bunge hilo la Katiba ambapo wamekuwa wakiweka vizuizi barabarani.

0 maoni:
Post a Comment