Kuandika
ujumbe na kupakia picha na video limekuwa jambo la kawaida kwa karibu
watu 1.8 bilioni wanaotumia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Ingawa ujumbe wako wa siasa au salama za heri, pongezi au rambirambi
unaweza kupendwa na wenzako, si wengi wanaoweka kuchukulia ujumbe huo
kuwa fasihi au kazi ya sanaa.
Lakini sasa Chuo Kikuu cha Delhi (DU) kimechukua msimamo tofauti.
Kinataka kujumuisha kuandika ujumbe wa Facebook kuwa sehemu ya mtalaa wake wa somo la Kiingereza.
Wanafunzi watakuwa wakifunzwa pia jinsi ya kuandika blogu au barua kuu ya kujitambulisha wakati wa kuwasilisha maombi ya kazi.
DU ni miongoni mwa vyuo vikuu bora zaidi nchini India.
Miongoni mwa waliowahi kusomea katika chuo kikuu hicho ni waziri mkuu
Narendra Modi na kiongozi wa Burma na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel
Aung San Suu Kyi.
Mambo hayo yamejumuishwa kwenye mswada wa mtalaa wa Kiingereza ambao unatathminiwa na maprofesa wa DU.
Prof Christel Devadawson, mkuu wa kitivo cha lugha ya Kiingereza
aktika chuo kikuu hicho, aliambia BBC kwamba ujumbe kwenye Facebook
utatumiwa kama sehemu ya Kozi ya Kuimarisha Ujuzi - ambayo ni sehemu ya
somo inayotumiwa kuwapa wanafunzi maarifa na ujuzi wa kuwawezesha kufaa
maeneo ya kazi.
Gazeti la Hindustan Times linasema nchini India, mitandao ya kijamii
inaweza kumzolea umaarufu mkubwa mwandishi chipukizi au msanii na
kumuwezesha kufikia watu wengi au hapa kupata matbaa ya kuchapisha kazi
zake.
0 maoni:
Post a Comment