Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) kupitia Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo
ya Nje, John Mrema wametuma salamu za rambirambi kufuatia kutokea kwa
ajali mbaya iliyotokea leo na kusababisha vifo vya watu 32.
Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje CHADEMA, John Mrema
Katika
salamu zao cha CHADEMA wamesema wamepokea taarifa hizo kwa masikitiko
makubwa kwani taifa limepoteza watu muhimu ambao wangelitumikia taifa
katika siku zijazo.
"Tumepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa za ajali mbaya Iliyotokea Leo tarehe 6 Mei,2017 Mkoani
Arusha, Wilaya ya Karatu na kusababisha vifo vya wanafunzi 33 (watoto wa
kike 16 na watoto wa kiume 17) waliokuwa wanafunzi wa Shule ya Lucky
Vicent ya Mkoani Arusha.....Hakika taifa limepoteza watoto wake na
vijana wa Kesho ambao wangelitumikia taifa letu siku zijazo". Alisema Mrema
Aidha, chama cha CHADEMA pia wametoa pole kwa familia ya wafiwa, uongozi wa shule ya Lucky Vicent pamoja na wananchi kwa ujumla.
"Kwa majonzi makubwa tunatoa salamu za pole kwa wazazi, wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent, uongozi wa Shule hiyo pamoja na wananchi wote wa Tanzania kwa msiba huu mkubwa na wenye kutia simanzi na huzuni kubwa...CHADEMA tutakuwa pamoja na familia za Marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo , tunawataka wanachama na watanzania wote bila kujali imani zetu tuwakumbuke wafiwa katika Sala /Dua ili Mwenyezi Mungu awatie ujasiri wafiwa katika kipindi hiki kigumu". Alisema Mrema

Pamoja na hayo, CHADEMA wamelitaka jeshi
la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha ajali hiyo mbaya
ili matokeo ya uchunguzi huo yatumike katika kuzuia ajali nyingine kama
isije kutokea katika siku zijazo.
0 maoni:
Post a Comment