Mbunge wa Kigoma mjini kwa
tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe na Chama Chake cha ACT Wazalendo
wametuma salamu za rambirambi kufuatia kutokea kwa ajali mbaya ya basi
dogo ambalo limepelekea vya wanafunzi 29, walimu 2 na dereva mmoja wa
gari hiyo.
Zitto Kabwe katika salamu zake za rambirambi anasema kuwa huu ni msiba mkubwa kwa taifa.
"Moyo wangu umesinyaa baada
ya kusikia Taarifa za ajali ya watoto wetu huko Karatu. Natoa salaam
zangu za rambirambi kwa Wazazi wa wanafunzi wa shule ya St. Lucky na Kwa
ndugu na familia za walimu na wafanyakazi wa shule waliopoteza maisha.
Huu ni msiba mkubwa sana. Huzuni haielezeki. Nawaombea Kwa Mola awape
wazazi na ndugu wote moyo wa subira katika mtihani huu. Ni msiba wa
Taifa zima" alisema Zitto Kabwe
Katika taarifa ya Chama Cha ACT Wazalendo pia imetoa pole kwa wanafamilia, walimu
"Chama cha ACT Wazalendo
kimepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa ya vifo vya wanafunzi,
walimu pamoja na wafanyakazi wa Shule ya awali na msingi ya Lucky Vicent
ya Jijini Arusha, vifo vilivyotokana na ajali ya basi iliyotokea katika
wilaya ya Karatu mkoani Arusha. ACT Wazalendo tunatoa pole kwa wazazi
waliopoteza watoto wao, ndugu na jamaa waliopoteza walimu na wafanyakazi
wa shule hiyo, pamoja na watanzania wote kwa ujumla. Pia tunawaombea
majeruhi wote wa ajali hii wapate kupona kwa haraka" alisema Abdallah Khamis Afisa Habari wa ACT Wazalendo
0 maoni:
Post a Comment