Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya wanafunzi 32 wa darasa la saba, walimu 2 na dereva wa gari la shule ya msingi Lucky Vicent ya Arusha vilivyotokea leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha ambapo wanafunzi hao walikuwa katika ziara yao ya masomo kuelekea shule ya msingi Tumaini kwa ajili ya kufanya mtihani wa ujirani mwema na walipofika katika eneo la Rhotia Marera basi walilopanda liliacha njia na kisha kutumbukia korongoni ambako limesababisha vifo hivyo na majeruhi watatu.