Mwanamuziki kutoka Marekani mwenye asili ya Morocco, Karim Kharbouch a.k.a French Montana ametoa msaada wa Dola laki moja nchini Uganda.
Montana ametoa msaada huo kwa taasisi ya Mama Hope nchini humo, pia ameanzisha kampeni inayojulikana kama Unforgettable Dance Challenge yenye lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya kusaidia jamii kuondokana na umaskini.
French Montana amenukuliwa akisema, “Muda mwingine Mungu anakupa uwezo wa kuwa sehemu fulani ili uwasaidie na watu wengine. Nataka niwape kile nilichonacho na kuwasaidia haraka iwezekanavyo.”
Kwa sasa Unforgettable ndio ngoma mpya ya msanii huyo aliyofanya Uganda na kushirikisha dance wa vijana Ghetto wa Uganda.
0 maoni:
Post a Comment