Rooney ameweza kucheza michezo 22 pekee katika michezo yote ya msimu huu ndani ya kikosi cha United, huku wakala wake akionekana nchini China mwanzo mwa Mwaka huu akijaribu kuzungumza na vilabu vinavyovutiwia na huduma ya mchezaji huyo.
Mchezaji wa Klabu ya Manchester United, Wayne Rooney.
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza ambaye ni mfungaji wa Muda wote, amesema anahitaji kusalia ndani ya kikosi cha Manchester United lakini hakuelezea atasalia katika kikosi hicho cha Mashetani wekundu mpaka lini.
Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa nusu fainali wa Europa League dhidi ya klabu ya Celta Vigo, Rooney amekiri kuwepo na maelewano mabovu kati yake na kocha wake Jose Mourinho.
Na alipoulizwa kuhusu maisha yake ya baadae na United amesema: “Nimekuwa katika klabu hii kwa takribani miaka 13 sasa, bila shaka nahitaji kucheza mpira.”
Na alipoulizwa kucheza “hapa” ? akajibu “Bila shaka.”
Rooney pia ameongeza kusema “Lengo langu ni kuisaidia United kuingia fainali za Europa League huko Stockholm, jambo ambalo itatupa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kama itashinda taji hili”.
“Kuna umuhimu mkubwa kwa sisi kurejea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya “ alisema. ” Kwa hali ilivyo, itakuwa vigumu kushiriki michuano hii kupitia Ligi, ila njia pekee iliyosalia ni kupitia kombe hili”.
0 maoni:
Post a Comment