Leo Celta Vigo wako Old Traford huku mashabiki zaidi ya 30,000 wakiwa wamesafiri na timu kutoka Hispania hadi Uingereza jambo linalompa faraja kocha wao Eduardo Berizzo.
“Ni faraja sana kwetu kwani inaonesha mashabiki hawa wako bega kwa bega na sisi, baada ya kufungwa mchezo wa kwanza hawajatuacha wamekuja na sisi hapa leo” alisema Berizzo.
Lakini Manchester United ambao wamerudi katika nafasi ya 6 kwenye ligi baada ya ushindi wa Arsenal hapo jana, watahitaji sana ushindi ili kucheza fainali ambayo inaweza kuwasaidia kushiriki Champions League msimu ujao.
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema ni muhimu sana kwao kama Manchester kushinda kombe hilo kwani ndio kombe pekee ambalo hawajawahi kulishinda.
“Hakuna aliyewahi kubeba kombe hilo hapa, nadhani itakuwa muhimu sana kwa wachezaji na timu kwa ujumla, hatupaswi kuwaza kuhusu mchezo uliopita bali tunapaswa kuwaza nini kinafuata” alisema Mourinho.
Katika mchezo mwingine Lyon ambao mchezo wa kwanza walikubali kipigo cha bao 4 kwa 1 toka kwa Ajax, leo watakuwa nyumbani kujaribu kubadili matokeo hayo.
0 maoni:
Post a Comment