Kupitia akaunti yake ya Instagram Nicki amepost picha inayomuonyesha yeye na rapa Nas wakiwa na ukaribu sana, jambo linalowapa maswali shabiki zake wakitaka kujua kuwa wawili hao ni wapenzi?.
Wawili hao walikuwa katika mgahawa anaomiliki Nas uitwao Sweet chick katika mji wa NYC, ambapo producer Statik Selekta naye alikuwepo na ndiye aliwapiga picha pamoja.
Nicki hajawahi kuficha upendo wake kwa Nas, na hata kufikia hatua ya kumshirikisha kwenye video yake ya ‘Right By My Side’ wimbo ambao unawaonyesha wawili hao wakiwa na hisia kali sana.
0 maoni:
Post a Comment