Shule zote katika kisiwa cha Zanzibar zimefungwa kwa muda kutokana na mvua kali ambayo imesababisha mafuriko.
Waziri wa elimu
katika kiswa hicho Riziki Pembe Juma amesema kuwa mvua hiyo ambayo pia
imekuwa ikinyesha katika kisiwa cha Unguja na Pemba kwa kipindi cha wiki
tatu zilizopita pia imeharibu barabara na mali ya watu.
Alisema kuwa
baadhi ya shule zimejaa maji hivyobasi kuwa vigumu kwa walimu kufunza
mbali na kuwa wanafunzi wanashindwa kufika kutokana na mafuriko.
Waziri huyo
amefichua kwamba uamuzi huo uliafikiwa kufuatia pendekezo kutoka kwa
kamati ya kukabiliana na majanga ya Zanzibar ambayo iliishauri serikali
kufunga shule hizo kwa usalama wa wanafunzi.
Baada ya
kuangazia mapendekezo hayo tulikuwa hatuna njia nyengine bali kuzifunga
shule hadi pale hali itakaporudia hali yake ya kawaida.
Hatahivyo amesema kuwa wanafunzi wa kidato cha sita waliokuwa wakifanya mitihani yao ya mwisho wataendelea kufanya hivyo.
Kufikia sasa kuna takriban wanafunzi 364 495 wa shule za msingi na zile za upili zanzibar.
0 maoni:
Post a Comment