Rais Uhuru
Kenyatta wa Kenya ametia saini muswada unaowaruhusu wakopeshaji kutumia
vifaa vya nyumbani mimea na mifugo ili kujipatia mikopo.
Sheria hiyo kwa
jina Movable Property Security Acto 2017 inatotoa fursa kwa kuanzishwa
kwa sajili ya kwa mali hiyo ambazo benki zinaweza kutumia kuthibitisha
umiliki dhamana yake.
Sheria hiyo mpya inalenga kuwasaidia wateja wa benki wasio na magari na vyeti vye umiliki wa gari ama hata ardhi kupata mkopo.
Sheria hiyo
inakuza uthabiti na uhakika kwa kutoa dhamana ya mali ,rais alisema muda
mfupi baada ya kutangaza kwamba ametia saini muswada huo.
Benki zimekuwa
zikikataa kutumia mali inayoweza kuhamishwa kama dhamana ya mkopo
kutokana na ukosefu wa data ambayo wanaweza kutumia ili kudai mali hiyo.
0 maoni:
Post a Comment