Takribani waumini 44 wameuwawa kwa kupigwa risasi wakiwa msikitini kaskazini mashariki mwa nigeria kwa mujibu wa maafisa wa jimbo la Borno.
mauaji ayo yalifanyika wakati wa maombi ya asubuhi jumapili ingawa taarifa zimejitokeza jumatatu,kutokana na itilafu ya mawasiliano kwani jimbo hilo liko chini ya sheria ya hali ya hatari.
shambulizi lilifanyika katika mji wa konduga ulio umbali wa kilomita 35 kutoka mji mkuu wa jimbo hilo maiduguli
washambulizi wamesema kuwa ni wana chama wa kundi la wapiganaji wa Boko Haram ambalo liliwauwa maelfu ya watu tangu mwaka 2009.
Raisi Goodluck jonathan alitangaza sheria ya hali ya hatari katika majimbo matatu kaskazini mashariki mwa nchi mnamo mwezi mei wakati wanajeshi walipo fanya operesheni dhidi ya wapiganajiwa kiislamu.
Boko Haram linapigania eneo la kaskazini mwa nchi likitaka kujitawala kwa kutumia sheria za kiislamu.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment