![]() |
| jijini Abuja |
Mwandishi wa JICHOPEMBUZI mjini Abuja Anthony Fuzu anasema milipuko iyo ilitokea wakati abiria wakiwa katika harakati za kupanda mabasi na teski wakienda maofisini katika mji wa Abuja.
watu walioshuhudia tukio hilo wanasema miili ya watu imepatikana katika eneo la tukio.
Waandishi wa habari wanasema huenda tukio hili ni shambulio la kikundi cha wapinaji wa kiislam kijulikanacho kama Boko Haram.
mmoja wa walioshuhudia mlipuko huo,Badamsi Nyanya ameiambia JICHOPEMBUZI kuwa ameona miili 40 ikiondolewa.
mlipuko huo ulichimba chini mita 1.2 katika viwanja vya Nyanya motor Park,kiasi cha kilometa 16 kutoka katikati ya jiji na kuaribu zaidi ya magari 30 na kusababisha mlipuko zaidi kutokana na matangi ya mafuta ya magari hayo kushika moto na kuwaka.

0 maoni:
Post a Comment