Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limepinga wito wa kulitaka liamishe dimba la Kombe la Dunia mwaka wa 2018 kutoka Urusi likisema kuwa kinyang'anyiro hicho "kinaweza kuleta mabadiliko makubwa"
Madai kuwa Urusi ilihusika katika kundungua ndege ya abilia ya malysia katika anga ya Ukraine yalizusha wito kutoka kwa wabunge nchini Ujerumani wa kutaka uwamuzi wa Urusi kupewa haki ya kuandaa Fainali hizo utathminiwe upya FIFA imetoa taarifa jana ikisema "linapinga aina yeyote ya machafuko"na inaunga mkono mdaharo wa amani na demokrasia pekee kuhusu kombe la Dunia.
Shirikisho hilo linasema historia kufikia sasa inaonyesha kuwa kususia matamasha ya michezo au sera ya kutenga au mapambano yasiyo njia bora za kutatua matatizo. badala yake kombe la dunia lina weza kutumiwa kama kitu kinacho weza kuchochea mazungumzo mwafaka baina ya watu na serikali husika.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment