Jeshi la Israel limesema kuwa limetoa onyo tena kwa wakazi wa mashariki na kaskazini mwa Gaza kuondoka majumbani mwao kwani wanaendeleza mashambulizi zaidi.
Onyo hili linajili wakati majaribio ya kusitisha mapigano katika eneo la palestina yakioneka kutibuka .
Maafisa wa jeshi wana sema maeneo mengi yanayo tumiwa kurusha maroketi kutoka Gaza yamelipuliwa huku kundi la Hamas likiendeleza mashambulizi ya roketi zidi ya Israel.
Habari za hivi punde zimesema hivi mashambulizi hayo ya Israel yamelenga na kupiga nyumba za viongozi wa ngazi za juu wa Hamas Mahmoud al-Zahar,na hile ya waziri wa zamani wa usalama wa ndani ya nchi fathi Hamad
Zaidi ya wapalestina 200 wameuawa katika mashambulio ya hivi sasa wengi wamejeruhiwa na huku majumba na miundombinu ya Gaza ikiwa imealibiwa sana Israel imedai kuwa imeongeza mashambulio kwani Hamas wamekataa majadiliano ya kidiplomasia.
Hata hivyo msemaji wa Hamas Osama Hamdan ameiambia JICHOPEMBUZI kuwa awaiamini Israel na hivyo awawezi kuzungumzia mpango wa Amani.wanao husikia tu kupitia vyombo vya habari kwani mpango huo awezi kamwe kuwasaidia wa- palestina.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment