SABABU ZA MZOZO WA GAZA UNAO UMIZA KICHWA DUNIA.

Ukanda wa Gaza ni kipande cha Ardhi kilichopo katikati ya Israel na Misri ,na eneo hilo limekuwa kitovu cha mzozo kati ya Israel na Palestina kwa miaka na miaka.

Israel iliikalia na kuidhibiti Gaza wakati wa vita vya mashariki ya kati vya mwaka 1967 ,na iliachilia eneo hilo kwa kuondoa majeshi yake na walowezi mwaka 2005 

Israel iliona hatua hiyo ni kama kumaliza kuikalia kimabavu Gaza,lakini bado inaendelea kudhibiti mipaka ya Gaza,inaendelea kudhibiti mfumo wake wa maji na pia inadhibiti anga za Gaza,Misri inadhibiti mpaka wa Gaza uliopo kusini

Israel iliweka sheria kali ya watu na bidhaa kutoka na kuingia Gaza,hatua anayo sema Israel ni muhimu kwa usala wake.

Hata hivyo wapalestina wanaona wanabanwa na kufungwa na wanaathilika na matatizo ya kijamii na kiuchumi.Makundi makuu ya wanaarakati wa palestina ,likiwemo kundi la Hamas wanasema hali ya Udhibiti haivumiliki.

Msimamo mkali wa Hamas ni kuiteketeza Israel,Ingawa kwa hivi karibuni imesema inatalajiwa kuwa na makubaliano ya amani na Israel ya muda mrefu.Hamas imesema israel kuendelea kukalia kimabavu maeneo ya ukingo wa magharibi na Jerusalem ya mashariki na ndio sababu ya kufanya mashambulio dhidi ya Israel,kabla na baada ya 2005.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment