MARAIS wa Jumuia ya Maendeleo ya nchi za Mashariki na pembe ya Afrika IGAD wanakutana leo mjini Addis Ababa Ethiopia kuujadili mzozo wa Sudan Kusini.
Mzozo huo nchini Sudan Kusini utibuka mwezi Desemba wapiganaji wanaounga mkono aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar walipozua vita dhidi ya Mejeshi ya Sudan Kusini mjini Juba.
Mkutano huu unawadia huku waasi wakishutumiwa vikali baada ya afisa mmoja wa uchunguzi wa IGAD kuuwawa katika hali ya kutatanisha mjini Bentiu.
Miongoni mwa viongozi ambao tayari wamewasili jijini Addis Ababa kuungana na mwenyeji wao Hailemariam Desalegn, ni rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni na Salva Kiir wa Sudan Kusini.
Mkutano huo ni juhudi ya hivi punde kutatua mzozo huo uliosababisha maafa mengi Sudan kusini.
Mazungumzo ya amani yanayoendelea jijini Addis Ababa, yamekwama kwa muda huku serikali ikisusia vikao kwa wiki kadhaa.
Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Dkt Riek Machar wametofautiana kuhusu serikali hiyo ya mpito.
Igad imeonya kuwa huenda ikachukua hatua za dhabu na kutangaza vikwazo dhidi ya viongozi wanaohujumu juhudi za kupatikana amani nchini humo.
Lakini hii si mara ya kwanza kwa Igad kutoa onyo kama hilo.
Mwezi Machi baada ya mkutano mwingine wa marais wa Igad, Mpatanishi mkuu wa mzozo huo Seyoum Mesfin alikuwa na onyo kama hilo hilo.
“ Mapigano yanaonyesha kwamba pande zote mbili hazina ari ya kumaliza vita.
NI ari yao ya kisiasa na ukakamavu ambao utamaliza vita hivi.
Kikao kimeweka bayana ujumbe wake, kwamba wakati huu ni lazima pande zote mbili ziitikie wito wa jamii ya kimataifa. “ alisema Mesfin
Wakati huohuo, Igad imeshutumu waasi nchii Sudan kusini baada ya mchunguzi wake mmoja kuuwawa.
Seyoum amesema waliohusika katika mauaji watachukuliwa hatua kali.
Mashirika ya misaada nayo yameonya kuwa nchini hiyo inakabiliwa na tishio la kiangazi huku vita vikitatiza utoaji wa chakula kwa mamilioni waliofurushwa makwao
0 maoni:
Post a Comment