Serikali na waasi kumaliza mazungumzo

 
Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Dkt Riek Machar
Rais wa Sudan Kusini Salva Kirr na kiongozi wa waasi Riek wamekubaliana kufanya mazungumzo ya kubuni serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa.
Mwenyekiti wa jumuiya ya ushirikiano wa kiserikali wa nchi za mashariki na pembe ya Afrika IGAD, waziri mkuu wa Ethiopia Hailemarriam Desalegne, amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa kwa lengo la kukomesha vita huko Sudan Kusini.
Baada ya mkutano wa zaidi ya saa nne katika ikulu ya waziri mkuu wa Ethiopia, mwenyeji wa mkutano huo Hailemarriam Desalegne alitangaza kuwa Kirr na mwenzake Machar wako radhi kushirikiana.
"Viongozi wa pande mbili, wamekubali kumaliza mazungumzo katika siku sitina zinazokuja, yatakayosababisha kuundwa kwa serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa", alisema Desalegne.
Ni kwa sababu hiyo vikao vitaanza Addis Ababa baina ya washirika wa Salva Kirr, Riek Machar na wale kutoka katika mashirika ya kijamii kujadili jinsi ya kuirejesha Sudan Kusini katika njia amani.
Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa viongozi hao wawili kukutana tangu watie mkataba wa kusitisha vita nchini Sudan Kusini.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment