Taasisi ya kimataiafa iliyojihusisha na tathmini juu ya ujenzi wa
Ukanda wa Gaza baada ya vita imesema itachukua muda wa miaka
20 kulijenga eneo hilo kufuatia vita kati ya wanamgambo wa Kundi la
Hamas na Israel. Tathmini hiyo iliofanywa na taasisi ya Shelter
Cluster,kwa kusimamiwa kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa
linalojihusisha na wakimbizi na Msalaba Mwekundu limeainisha
ugumu wa ujenzi wote wa Ukanda wa Gaza, ambao baadhi ya
maafisa wa Palestina wanakadiria utaghalimu kiasi cha dola bilioni 6.
Jitihada zozote za kuijenga upya Gaza zitakwamishwa na mzingiro
uliowekwa na Misri na Israel tangu wanamgambo wa Hamas,
kuchukua madaraka ya eneo hilo 2007. Israel imeweka vizuizi vikali
katika uingizwaji wa saruji na vifaa vingine vya ujenzi mjini Gaza, kwa
kuhofia wanamgambo watavitumia katika kutengeneza maroketi na
kujiongezea uwezo katika mashambulizi yao ya kuvuka mipaka.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment