KESI YA BUNGE LA KATIBA KUTAJWA SEPTEMBA 4.

Ombi la kuiomba mahakama kuu nchini tanzania etoe amri ya kusimamisha bunge maalumu la katiba lililofunguliwa na mwandishi wa habari Saed kubenea litatajwa septemba 4 na kuanza kusikilizwa septemba 15 katika mahakama kuu kanda ya Dar es salaam 

Ombi hilo linatarajiwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu likiongozwa na jaji Augustine mwarija wengine ni jaji Dk Fauz Twaib na Jaji Aloysius mujuluz 

Kubenea aliwasilisha ombi hilo mwishoni mwa wiki hiliyo pita dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali kupitia kwa wakili wake peter kibatala akiomba bunge hilo lisimamishwe hadi mahakama itakapo toa tafsiri sahihi ya bunge hilo kuhusu mamlaka iliyonayo na kama ni sahihi kwenda kinyume na Rasimu.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment