UINGEREZA YAONYA KUHUSU MASHAMBULIZI YA WANAJIHADI WA ISLAMIC STATE (IS)

Serikali ya uingereza imesema kuwa matukio yanayo shuhudiwa nchini Iraq na Syria yameongeza tishio ya kufanyika kwa mashambulizi ya kigahidi nchini Uingereza.

Waziri mkuu wa uingereza Devid Cameron amewaambia waandishi wa habari kuwa hakuna shaka kwamba wanajihadi wa kundi la Islamic State lililopo nchini Iraq na Syria kwa sasa linapanga kufanya mashambulizi katika nchi za Ulaya.

Kiwango cha tishio hilo kimeongezeka kutoka kuwa kikubwa hadi kuwa kibaya zaidi wakati huu umoja wa mataifa ukisema idadi ya wakimbizi kutoka syria imeongezeka na kufikia milioni tatu.

Raia milioni tatu kutoka Syria wanalipotiwa kuyahama makazi yao,baadhi wamekimbilia nje ya nchi kufuatia mapigano yanayo endelea kati ya jeshi la Syria na waasi wanao pinga utawala wa Bashar Al Assad ambapo shirika la umoja wa mataifa  linalo udumia wakimbizi UNHCR limebaini kwa linahitaji Dola bilioni 2 hadi mwishoni mwa mwaka 2014 hili kuwaudumia wakimbizi hao.

Hata hivyo,Tangu kuzinduliwa kwa mfumo mpya wa kuwataadharisha raia mnamo mwaka 2006Uingereza imekuwa ikitishiwa na shambulizi la kigaidi kwa takribani miaka minne na tishio hili ni la tatu kwa ukubwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment