Mtoto Rose (kushoto) aliyelawitiwa, na mwenzake Diana aliyetoroshwa na kigogo mmoja aliyetajwa kwa jina la Moses.
INASIKITISHA sana!
Wakati watetezi wa haki za binadamu wakizidi kupiga vita matukio ya
unyanyasaji wa watoto na wanawake, kigogo mmoja aliyetajwa kwa jina la
Moses anadaiwa kumlawiti mtoto, Rose (16) na kumtorosha mwingine aitwaye
Diana (12) ambaye ni denti wa darasa la nne.
Kigogo huyo anayesemekana kuwa ni mfanyakazi wa taasisi moja ya serikali
iliyopo jijini Dar (jina tunalihifadhi) alidaiwa kumfanyia kitendo
hicho mtoto huyo ndani ya shamba lake.
Tukio hilo lilitokea Agosti 20, mwaka huu maeneo ya Zogowale, Kibaha
Pwani ambapo wachunga ng’ombe waliwaona watoto hao wakiwa katika banda
peke yao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti hivi karibuni, walisema walitolewa
mkoani Lindi kwa ajili ya kufanya kazi za ndani huku Diana akianika
kwamba huyo Moses alimlaghai kuwa angemnunulia nguo jambo ambalo
hakulifanya.
“Mimi nilichukuliwa mwaka jana na kupelekwa Dar kwa ajili ya kufanya
kazi za ndani, baadaye Moses alinitoa na kunihamishia hapa shambani
kwake bila kufanya mawasiliano na wazazi wangu kwani sikuwaaga wakati
nakuja,” alisema Rose.Akaongeza: “Nilishindwa kuwaambia wazazi wangu kwa
sababu alininyang’anya simu halafu akaanza kunilawiti.”
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Jonunga, Mbegu Twaha alisema taarifa za
watoto hao alizipokea kutoka kwa wachunga ng’ombe hao hivyo akaamua
kwenda kwenye shamba hilo na kuwakuta bandani.
Alisema baada ya kufanya mahojiano na watoto hao alibaini kuwa, Rose
alikuwa akilawitiwa na bosi wake, ndipo akaamua kwenda kutoa taarifa
katika Kituo cha Polisi Mlandizi kwa ajili ya fomu ya matibabu (PF3)
ambayo ilionesha kuwa kweli binti huyo alikuwa akiingiliwa.
kwa ushirikiano na viongozi wengine wa kijiji walifanikisha kuweka
mtego kumnasa mtuhumiwa huyo na kufikishwa polisi ambako alifunguliwa
jalada la kesi lenye Kumbukumbu Na. MLA/IR/1066/2014 KULAWITI.
0 maoni:
Post a Comment