Mhe. Meya
Wills akipokelewa na Bw.Suleiman Saleh, Afisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya
Muungano waTanzania, Washington DC mara baada ya kuwasili Ubalozini hapo
kwa mazungumzo na Mhe. Balozi Liberata Mulamula
Mhe. Balozi Mulamula akimkabidhi Meya Wills zawadi maalum kutoka Ubalozini.
.Mhe. Mulamula akiwa katika picha ya kumbukumbu na Mstahiki Meya Wills wa Mji wa Helena –West Helena, Arkansas, Marekani.
Balozi wa
Jamhuri ya Muungano nchini Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula jana
Jumanne Agosti 26, 2014, alikutana na Mhe. Mstahiki Meya wa Mji wa
Helena-West Helena kutoka jimbo la Arkansas, Marekani, Ubalozini “Tanzania House” Washington
DC. Mhe. Wills ambaye Mji wake wake wa Helena-West Helena una
mahusiano ya kidada (Sister City) na Mji wa Moshi, Tanzania, alifika
Ubalozini ili kufahamiana na Mhe.Balozi Mulamula pamoja na kumuelezea
mashirikiano yaliyopo baina ya Mji wa Helena-West Helena na Moshi ambapo
makubaliano rasmi yalisainiwa Oktoba 12, 2012, hapa Marekani kufuatia
ziara ya Mhe. Japhary Michael, Meya wa Mji wa Moshi katika mji wa Helena
–West Helena, Arkansas.
Katika
mazungumzo hayo Mhe. Wills alimuelezea Mhe. Balozi Mulamula juhudi zake
katika kuimarisha mashirikiano hayo ya miji hiyo miwili ambapo
yamejikita zaidi katika sekta ya utalii pamoja na shughuli nyingine za
kukuza uchumi. Balozi Mulamula alimshukuru Meya Wills kwa kumtembelea na
kufurahishwa na Meya huyo kutokana na kutembelea Tanzania mara mbili na
kupata ufahamu zaidi wa Tanzania na hivyo kusaidia kupanua mahusiano
yaliyopo baina ya Moshi na Helena –West Helena. Mhe. Mulamula alimshauri
Mhe. Meya Wills kupanua wigo wa ushirikiano huo katika sekta nyingine
za uchumi, biashara na uwekezaji.
0 maoni:
Post a Comment